Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Vincent Mashinji, Mbunge wa Ndanda Cecil Mwambe ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kusini pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma Zubeda Sakuru wanashikiliwa na Polisi wilayani Mbamba Bay.
Polisi wamewakamata Dkt. Mashinji, Mbunge Mwambe na Mbunge Zubeda baada ya kuvamia kikao cha ndani kilichokuwa kikiendelea ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu huyo kukagua shughuli za chama katika majimbo ya Kanda hiyo iliyoanza leo.
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Mashinji, Wabunge Cecil Mwambe na Zubeda Sakuru wamekamatwa na kuhojiwa na polisi kuhusu kuwepo kwao Mbamba Bay. pic.twitter.com/Mps2Y2rulU
— millardayo (@millardayo) July 15, 2017
Muda ulioongezwa na TRA kulipia kodi za majengo!!!