Taarifa iliyotolewa leo December 20, 2017 kuhusu yaliyojiri katika Kikao Cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) baada ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa 9, imeeleza kuwa Rais Magufuli ameunda Tume ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) itakayokuwa na jukumu la kwenda kufuatilia mali za chama hicho kote nchini Tanzania.
Kikao hicho cha NEC cha kwanza chini ya JPM kimeanza kazi kwa majadiliano juu ya mikakati ya kuimarisha kazi za Chama hicho na serikali. Akitoa maelekezo kwa wajumbe wa NEC amewataka kutambua wajibu wao.
“Tumekuwa viongozi kwa sababu Mungu amependa tukafanye kazi,tukatende haki, tusiwaonee watu, tukatimize wajibu wetu, tukasimamie maadili ya chama,” – JPM
Katika mkutano huo President JPM ameunda Tume ya Chama cha Mapinduzi itakayokuwa na jukumu la kufuatilia Mali za chama hicho kote nchini.
Wafuatao wameteuliwa katika Tume ya CCM ya kufuatilia na kuhakiki Mali za Chama hicho; –
1. Dkt. Bashiru Ali Kakurwa – Mwenyekiti wa Tume
2. Walter Msigwa – Mjumbe
3.Albert Msando – Mjumbe
4.Galala Wabanhu (Hananasif) – Mjumbe
5. Albert Chalamila – Mjumbe
6. William Sarakikya – Mjumbe
7. Komanya Kitwara – Mjumbe
8. Dkt. Fenela Mkangara – Mjumbe
9. Mariam Mungula – Mjumbe
“SITAKI KUONGEA MENGI, TUMEBANA VYUMA VILIVYOLEGEA” -JPM, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA