Abiria zaidi ya 80 waliotakiwa kusafiri na ndege ya shirika la ATCL kwenda Comoro wamekwama kusafiri baada ya Ndege ya Shirika la ATCL waliyotakiwa kusafiri nayo kuharibika.
Shirika la ATCL wamesema ndege ilipata tatizo la kiufundi na tayari spare zimeingia nchini na utengenezaji unaendelea na watawasafirisha siku ya alhamisi na ikishindikana watawasafirisha kwa ndege ya shirika lingine. Shirika hilo lina ndege moja ambayo inafanya safari zake za Dar es salaam na Comoro.
Kwenye video hii fupi hapa chini ni mmoja wa abiria aliyetakiwa kusafiri na ndege hiyo ameyazungumza haya……>>> ‘tunakaribia wiki mbili kila siku tunakuja wanatuambia nendeni mtakuja tena, mpaka leo hatujui mpaka lini tutaondoka’
Kwenye video fupi hapa chini ni Kaimu afisa mawasiliano ATCL, Lily Fungamtama ambaye ameyazungumza haya ….>>>’ili kurekebisha ndege iweze kuruka, inaweza kuchelewa au ikawahi kwa hiyo tumefanya utaratibu wa abiria wetu ambao tumewaacha waondoke alhamisi’
#UPDATE2 Shirika la ATCL limesema ndege ilipata tatizo la kiufundi na watawasafirisha abiria wa Comoro alhamisi pic.twitter.com/0L4tPzro5V
— millardayo (@millardayo) May 17, 2016
ULIPITWA NA MAAMUZI YA WAZIRI WA UCHUKUZI BAADA YA MILIONI 700 KUPOTEA MILIONI 700? BNYEZA PLAYA HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE