Ni mara ngapi tumesherehekea siku za kuzaliwa za Watu wetu na zetu wenyewe alafu mishumaa ikajazwa kama yote kwenye keki za birthday ili kunogesha keki na tukio lenyewe? ukweli ni kwamba inaweza kuwa ni mara nyingi tumefanya hivyo… sasa leo kuna hizi ripoti za utafiti tumeletewa.
Ripoti yenyewe inasema imegundulika kwamba kuwasha mishumaa kwenye keki kunasababisha keki yenyewe kuwa na bakteria kama 1400 ambao huweza kusababisha magonjwa kwa Binadamu.
Utafiti huu ambao umechapishwa kwenye Journal of food unasisitiza kuwa bakteria hawasababishwi na mishumaa tu ila hata mvuke unaotoka kinywani wakati wa kuzima mishumaa nao huongeza bakteria kwenye cake.
Mamilioni ya Watu duniani husherehekea siku za kuzaliwa kila siku ambapo kwa hapa Tanzania pia kadri siku zinavyozidi kwenda ndio Biashara ya utengenezaji keki inazidi kuongezeka na mtindo mpya wa sasa umekua rahisi zaidi kwani unaweza kupiga simu ukatengenezewa na ukaletewa ulipo hivyo hauwezi kufahamu mazingira ya utengenezaji keki yalikuaje hadi kukufikia wewe.