Atletico Madrid imemsajili fowadi wa Argentina Julian Alvarez kutoka Manchester City ya Ligi Kuu ya Uingereza kwa mkataba wa miaka sita, klabu hiyo ya La Liga ilisema Jumatatu.
Taarifa za kifedha kuhusu uhamisho huo hazikufichuliwa na klabu zote mbili, lakini vyombo vya habari vya Uingereza viliripoti kuwa mkataba huo ulikuwa na thamani ya euro milioni 75 ($82 milioni) pamoja na euro milioni 20 kama nyongeza zinazowezekana.
“Leo naiaga klabu hii nzuri yenye hisia nyingi. Ilikuwa miaka miwili ya kipekee sana. Wakati huu, nilikua na kujifunza mengi kama mchezaji na kama mtu,” Alvarez alisema kwenye Instagram.
“Siku zote nitajivunia kuwa sehemu ya familia hii, Manchester City daima itakuwa na nafasi maalum moyoni mwangu. Nawatakia kila la kheri katika siku zijazo na nitaendelea kuisapoti klabu popote nilipo.