Polisi wa Australia wanashirikiana na wenzao kimataifa kumtafuta Mwanaume anayeshukiwa kutoroka Nchi baada ya kumwagia Mtoto wa miezi tisa kahawa ya Moto mjini Brisbane.
Shambulizi hilo la kiholela, lililotokea mwezi uliopita, limemwacha Mtoto huyo na majeraha makubwa usoni na mikononi, Polisi wa Queensland wametoa hati ya kukamatwa kwa Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 33 kwa kosa la kutenda vitendo vinavyokusudia kuleta madhara makubwa, ambalo linaweza kupelekea kifungo cha Maisha.
Hata hivyo, Polisi walisema kuwa mshukiwa huyo aliondoka Nchini kwa ndege kutoka Uwanja wa ndege wa Sydney siku sita baada ya tukio hilo, na masaa 12 kabla ya kuthibitisha kitambulisho chake, Mtoto huyo alikuwa akicheza na familia yake kwenye Mbuga ya Jiji tarehe 31 Agosti, wakati mashahidi wanasema Mwanaume huyo alimsogelea Mtoto huyo na kumwagia kahawa ya Moto kabla ya kutoroka kwa miguu.
Mchunguzi Mkuu Paul Dalton, alisema Polisi wanafahamu Nchi aliyokimbilia mshukiwa pamoja na jina lake, lakini ufunuo wa maelezo haya unaweza kuhatarisha uchunguzi. Mshukiwa ni Mfanyakazi anayesafiri ambaye amekuwa akitembea mara kwa mara Nchini Australia tangu mwaka 2019 na alikuwa na anwani New South Wales na Victoria. Aidha, Mchunguzi Dalton alisema mshukiwa alikuwa akijua mbinu za polisi na alikuwa akifanya shughuli za kupambana na uchunguzi ili kuepuka kukamatwa.
Aidha Wazazi wa Mtoto walipokuwa wakiongea na vyombo vya habari walieleza kuwa wamepigwa na bumbuazi kutambua kuwa mshukiwa alikimbia Nchi lakini walifurahi kwamba sasa hayupo.
“Inaonekana walikuwa karibu kumkamata, na hii inamaanisha kwamba tutalazimika kusubiri muda mrefu kupata haki kwa Mtoto wetu,” alisema mama wa Mtoto, Mtoto yupo katika hali nzuri, baba aliongeza, lakini huenda akahitaji upasuaji wa ngozi zaidi.
Kurasa ya GoFundMe kwa ajili ya Mtoto huyo imekusanya zaidi ya A$150,000 (takriban $100,000).