Australia itaharakisha juhudi za kununua makombora ya masafa marefu ili kukabiliana na tishio linaloongezeka kutoka Uchina,tathmini muhimu ya Ulinzi imesema.
Inaonya kuwa nchi haiwezi kulindwa tena na kutengwa kwake kijiografia katika “zama za makombora”.
Serikali itatumia dola za Australia $19 bilioni ufanya ununuzi huo wa haraka na ripoti hiyo ya kurasa 110 inaelezewa kama marekebisho makubwa zaidi ya ulinzi wa Australia tangu Vita vya Pili vya Dunia.
Waziri Mkuu Anthony Albanese alisema Mapitio ya Mkakati wa Ulinzi (DSR) yaliyosubiriwa kwa muda mrefu ni “kazi muhimu zaidi ambayo imefanywa tangu Vita vya Pili vya Dunia… [katika] ulimwengu ambapo changamoto kwa usalama wa taifa letu zinaendelea kubadilika”.
Tathmini hiyo inakuja huku kukiwa na ongezeko la mvutano wa kijeshi katika kanda hiyo kuhusu msimamo wa China kuelekea Taiwan, ambayo imeapa mara kwa mara kuichukua kwa nguvu ikibidi.
Jeshi la wanamaji la China pia limeanzisha uwepo mkubwa katika Bahari ya China Kusini, likidai sehemu zake kama eneo lake, kinyume na sheria za kimataifa.