Kimbunga kimeua watu tisa kwenye pwani ya mashariki ya Australia, mamlaka imetangaza leo Jumatano, eneo ambalo zaidi ya nyumba 80,000 zimesalia bila umeme.
Waliofariki, akiwemo msichana wa umri wa miaka tisa, walikuwa katika majimbo ya Queensland na Victoria, yaliyokumbwa na radi na upepo mkali tangu Jumatatu, na kusababisha kuanguka kwa miti na mafuriko.
Boti iliyokuwa na watu kumi na moja ilipinduka karibu na Brisbane, na kusababisha vifo vya wanaume watatu kwa kuzama, imesema polisi, ambayo imepata maiti ya tatusiku ya Jumatano.
Wafanyakazi wengine wanane iongoni mwa wafanyakazi wa boti hili, ambao walikuwa katikati ya safari ya uvuvi, walisafirishwa hadi hospitali.
“Saa 24 zilizopita zimekuwa mbaya kutokana na hali ya hewa,” Mkuu wa Polisi wa Queensland Katarina Carroll amewaambia waandishi wa habari.
Huko Gympie (mashariki), wanawake wawili waliuawa baada ya kudondoka kwenye shimo kubwa la maji ya mvua, na mwanamke wa tatu, ambaye alinusurika, vikosi vya polisi vimesema.