Kijana mwenye umri wa miaka 14 amewaka moto baada ya kugusa nyaya za juu kwenye Treni ya umeme ya kubebea mizigo Nchini Urusi, jambo lililosababisha ajali mbaya.
Katika tukio hilo, video iliyosambaa Nchini humo inayoonyesha kijana huyo akipatiwa na mlipuko mkubwa wa moto ulipokutana na mwili wake, huku nywele na mavazi yake yakichomwa moto.
Ingawa iliripotiwa awali kuwa alikufa papo hapo, maokozi walipofika waligundua kuwa bado anaishi na walimkimbiza hospitali katika kijiji cha Arctic cha Shonguy, kilichoko katika Mkoa wa Murmansk, hadi sasa, amekuwa akipatiwa matibabu katika wodi ya wagonjwa mahututi, huku akielezwa kuwa ana fahamu.
Kijana huyo alipata “majeraha makubwa baada ya kuchomwa na umeme,” kulingana na ripoti za Plokhie Novosti kiijana mmoja aliyekuwapo na kushuhudia tukio hilo kwa hofu na alifunika uso wake kwa mikono yake alipoona kilichotokea.
Aidha, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Usafiri wa Murmansk inachunguza tukio hilo, huku mamlaka Nchini Urusi zikionya mara kwa mara kuhusu hatari za kupanda Treni.