Mbali ya Gerrard pia Mshambuliaji kinda Raheem Sterling ametajwa kama mchezaji bora chipukizi wa mwaka kwenye klabu hiyo licha ya baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo kumzomea kwa kitendo chake cha kytaka kuihama timu hiyo huku Philippe Coutinho akitajwa kama mchezaji bora wa mwaka.
Baada ya kupokea tuzo hiyo nahodha huyo aliwashukuru makocha wake pamoja na wachezaji wenzake kwa ushirikiano waliouonyesha kwa kipindi chote alichoichezea klabu hiyo.
Kwa upande wa Manchester United pia walitoa tuzo kwa wachezaji wao ambapo kipa David de Gea anayetajwa kutaka kuhamia Real Madrid alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Manchester United na mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Hispania, Juan Mata ameshinda tuzo ya bao Bora la Msimu alilofunga katika mechi dhidi ya Liverpool.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.