Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga kuipa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (Dawasa), Sh milioni 500, ili mamlaka hiyo ikamilishe kazi ya kuunganisha mai kwa wananchi wa Jimbo la Kawe wanaohudumiwa na mradi wa maji wa Mapinga Bagamoyo, Mbweni na Tegeta A.
Aweso ametoa maagizo hayo leo Desemba 21, 2022 alipowasha pampu ya maji ya Mapinga hadi Changanyikeni yenye urefu wa zaidi ya kilomita 1,225, ambao ujenzi wake umegharimu zaidi ya Shilingi bilioni 70.
Amesema uwekezaii uliofanvika ni mkubwa na kwamba dhamira ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha watu wote wanapata maji.
Pia Aweso ameitaka Dawasa kuwaunganishia wateja maji ndani ya siku saba tangu wanapotuma maombi.
“Mteja anapoomba kunganishiwa maj§ maji ndani ya siku saba awe ameshapata maji, sio danadana nyingi, na nitalifuatilia hili,” amesema.