Mbunge wa Pangani, Tanga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso ametumia ukurasa wake wa Instagam kufikisha hisia zake baada ya Serikali kutoa kibali cha ujenzi wa barabara ya Pangani ambayo kihitoria imekuwa ni kikwazo kwa watangulizi wote wa nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo na kusababisha Wananchi kutokuwa na imani nao kwa kigezo cha kushindwa kufanikisha ujenzi wa barabara hiyo.
Aweso ameandika ujumbe uliosomeka >>>“Ndugu zangu Nina furaha sana huenda zaidi ya siku zote ukitoa siku niliopata ridhaa ya kuaminiwa na wana Pangani kua Mbunge wao.Asanteni sana.!“
“Kitu kinachoifanya siku hii ya leo kua ya kipekee sana ni BARABARA yetu ya PANGANI kupewa kibali rasmi cha matengenezo toka kwa Mh.Raisi wetu Mpendwa Dk.John Pombe Magufuli na hapa nimefika ofisini kwa Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu Dodoma kujionea na kushukuru.“
“Ndugu zangu kila kilio kina mwenye ,;machozi ya furaha yamenitoka nilipopewa habari hizi,nimekumbuka mbali sana tulivyoumia, tulivyoteseka pamoja na kwa miaka mingi sana kusubiri hili.“
“Hisia zimenipeleka mbali nilivokosa amani toka nilipopata ridhaa ya kua Mbunge namna nimekosa usingizi kila nikiwaza kulimaliza na kufanikisha hili,nilifikia hatua kila nikisimama Bungeni nasemea barabara tu,nilipiga mpaka MAGOTI kwa Waziri Mbalawa alipofika Pangani,nimeenda ofisi zote hamna sehemu sijafika kuisemea barabara hii,nimetembelea Media mbalimbali.,nimemuomba sana Mungu kila nifapo Dua.!“
“Leo ni siku ya kihistoria ninaomba kuwajulisha rasmi kua tunaenda kupata barabara ya kiwango cha lami na zoezi hili litaanza muda si mrefu.
Tumesema sana,tumepaza sauti kila kona,tumezungumza na kila aliehusika na sasa faraja kubwa hii hapa Mbele yetu.”
“Nichukue nafasi hii kuwashukuru sana wana Pangani kwa uvumilivu wenu kipindi chote nilipowaambia naipambania barabara hii,na niwaombe tuendelee kua na subira mpaka mchakato unapoanza,nawashukuru sana kwa Dua zenu na nawaomba uzidi kuniombea nina mengi ya kufanya kwa ajili yenu.“
“Mwisho nikiri nimeupokea utendaji wa Mh.Raisi wetu wa Miaka mitatu kwa moyo wa furaha sana na Mungu ampe nguvu na Afya na maisha marefu tokana na hiki kilio cha muda mrefu kinachokwenda kufutika ikiwa ni kama Pangani tulikua pangoni sasa tunaenda kupaa angani.!”
BULEMBO AMPA MUSIBA SIKU 7 “SIWEZI KUCHONGANISHWA NA MAGUFULI“