Kiungo wa kimataifa wa Ghana na klabu ya Marseille ya Ufaransa, Andre Ayew amefanikiwa kuwashinda wenzake Max Alain wa Ivory Coast, Aymen Abdennour wa Monaco pamoja na Saint Etienne kutoka Tunisia na kushinda tuzo.
Kiungo huyo ambaye ameisaidia timu yake ya Taifa kwa mafanikio makubwa amefanikiwa kushinda tuzo ya mwanasoka bora kutoka Afrika katika ligi kuu ya Ufaransa.
Akiwa na miaka yake 25 aliisaidia kwa kiasi kikubwa Ghana katika mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika mw aka huu na ilifungwa na Ivory Coast kwa penalti ya 9-8 kwenye mchezo wa fainali.
Ayew amefanikiwa kufunga magoli 10 katika mechi 27 alizocheza na anatarajia kuachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu huku kukiwa na tetesi huenda akaenda katika moja ya klabu za ligi kuu ya England msimu ujao ikiwemo Arsenal, Man United, Liverpool na Newcastle.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.