Asubuhi ya July 13 2016 nilianza kuona naandikiwa msg na wengine kuniandikia kwenye mitandao ya kijamii kwamba kumetokea tetemeko la ardhi kwenye mkoa wa Dodoma na mpaka wengine wakaelezea walivyopata na hofu.
Sasa ili kujua kama kuna madhara yoyote yaliyotokea kwenye maeneo mbalimbali ya Dodoma lilikopita tetemeko hilo, millardayo.com imempata Kamishna msaidizi wa Polisi Lazaro Benedict.
Amesema ‘ni Kweli tetemeko limetokea asubuhi hii lakini hakuna madhara yoyote yaliyoripotiwa sehemu yoyote, ilikuwa ni majira kati ya saa kumi na mbili asubuhi kuelekea saa moja kamili asubuhi’
ULIIKOSA HII YA NAIBU SPIKA KUHUSU MBUNGE JOSEPH MBILINYI KUONYESHA ALAMA YA KIDOLE KAMA TUSI BUNGENI? BONYEZA PLAY HAPA CHINI