Mwanaharakati wa Tanzania wa kupinga ndoa za utotoni, Rebeca Gyumi ambaye ni Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali, Msichana Initiative linalotetea haki za wasichana kupata elimu ameshinda tuzo ya umoja wa Mataifa inayotolewa kupitia UNICEF katika kipengele cha mabadiliko ya kijamii.
September 23 2016 amewasili nchini kutokea Marekani na kupokelewa kama mshindi wa tuzo ya umoja wa mataifa kupitia UNICEF katika kipengele cha mabadiliko ya kijamii
‘Kwa kweli nimefurahi sana japokuwa tuzo hizi zilikuwa ni chache ila ninachojivunia ni kuwa nchi yangu ya Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi zizilizopata tuzo hizi, ninachoona sasa hivi kama jamii tufikiri zaidi jinsi gani ya kuwekeza kwa watoto na sio tena kuwaozesha katika umri mdogo‘>>>Rebeca Gyumi
ULIKOSA HII YA REBECCA GYUMI BAADA YA KUSHINDA KESI YA KUPINGA NDOA ZA UTOTONI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI