Benki ya NMB wameshirikiana na timu ya Azam FC jana na kuzindua rasmi kadi za wanachama wa klabu hiyo ambazo zitawawezesha kupata huduma za kibenki za NMB.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, aliwataka wanachama kuitumia huduma hiyo iliyoboreshwa na pia kuwa tayari kuiunga mkono timu yao kwa matokeo yoyote.
Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Barnabas Waziri alisema kuwa NMB itaendelea kushirikiana na Azam kukuza mpira hapa nchini na vile vile kuhakikisha kwamba mashabiki wa mpira wanapata nafasi ya kupata huduma za kibenki kwa urahisi na karibu zaidi.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook