Baada ya April 9 klabu ya Yanga kucheza mchezo wake wa klabu Bingwa Afrika dhidi ya klabu ya Al Ahly ya Misri na kutoka sare ya goli 1-1, Jumapili ya April 10 ilikuwa zamu ya Azam FC kuiwakilisha Tanzania dhidi ya klabu ya Esperance ya Tunisia katika mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Azam FC wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Azam Complex walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1, klabu ya Esperance ya Tunisia ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 34 kupitia kwa Haithem Jouini, goli la Esperance liliwafanya Azam FC kuchanganyikiwa.
Mambo yalibadilika kipindi cha pili baada ya kocha wa Azam FC Stewart Hall kuongea na vijana wake wakati wa mapumziko, Azam FC walirudi na mbinu mpya hatimae Farid Mussa akachomoa goli dakika ya 68 na dakika ya 70 Ramadhani Singano akapachika goli la ushindi kwa Azam FC. Matokeo hayo yanawafanya Azam FC kutafuta sare ya aina yoyote katika mchezo wao wa marudiano.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE