Mfanyabiashara maarufu nchini Rostam Aziz amevunja ukimya juu ya ushabiki wake kwa klabu ya Yanga ambapo amesema kuwa amekuwa akiishabikia timu hiyo kwa kipindi kirefu na kwamba amekuwa akiisaidia kimya kimya.
“Nimekuwa nikiichangia Yanga kimyakimya sasa nilivyochangia hadharani katika harambee ya juzi watu wakaanza kuzungumza maneno mitandaoni” Rostam Aziz
“Timu kama Yanga haitakiwi kumilikiwa binafsi na haitakiwi kuwa na Mfadhili kwa sababu ni timu ya Mamilioni ya watu na unapokuwa na mtu binafsi anamiliki timu muhimu yenye historia kama hii inawanyima wanachama Mamilioni sauti muhimu ktk klabu yao” Rostam Aziz