Usiku wa April 27 2018 millardayo.com imezipata taarifa za kifo cha mdogo wa Mbunge wa Tarime John Heche anayeripotiwa kupoteza maisha kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali.
Mdogo wa wa mbunge huyo anayejulikana kwa jina la Chacha Heche Saguta mwenye umri wa miaka 26, anadaiwa kuuwawa na askari Polisi ambaye kwa sasa anashikiliwa na Polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya.
Jeshi la Polisi linamshikilia askari wale koplo William Marwa mwenye namba E 1156 kwa tuhuma za kusababisha kifo cha kijana Chacha Heche Saguta, millardayo.com inaendelea kufuatilia taarifa hizi kwa kina.