Club ya Dar es Salaam Young Africans licha ya kudaiwa kutokuwa katika hali nzuri kiuchumi kwa sasa toka aondoke mwenyekiti wao Yussuf Manji, ila mambo yanadaiwa kuendelea vizuri zaidi pamoja na kudaiwa kuwa na ukata, Yanga ikicheza dhidi ya Biashara United ya Musoma imeendeleza kulinda rekodi yake ya kutopoteza mchezo.
Yanga ikiwa nyumbani uwanja wa Taifa imefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 2-1, magoli ya Yanga yakifungwa na Abdallah Shaibu dakika ya 70 na Heritier Makambo aliyefunga goli la ushindi, Yanga walilazimika kusubiri hadi dakika 70 ndio wafunge goli la kusawazisha, kwani Bishara walikuwa wanaongoza kwa goli moja lililokuwa limefungwa na Abdulmajid Mangola dakika ya 38 ya mchezo.
Ushindi huo umeifanya Yanga kuendelea kuwa kinara wa TPL msimu huu wakiwa na jumla ya point 41 walizovuna katika michezo 15, huku Azam FC ikiwafuatia kwa karibu kwa tofauti ya point 2 wakati Azam FC wakiwa na point 39 na Simba wakiwa nafasi ya tatu kwa kuwa na point 27 na viporo vitatu, kipigo hicho kwa Biashara United kinazidi kuididimiza baada ya kuiweka mkiani ikiwa na point 10.
MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe