Club ya Simba SC kupitia ukurasa wake rasmi wa instagram umeandika taarifa kuwa club hiyo imelazimika kumsafirisha mshambuliaji wake John Rafael Bocco kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya misuli.
John Bocco kwa zaidi ya miezi miwili sasa amekuwa nje ya uwanja kwa sababu ya kusumbuliwa na misuli, hata hivyo Bocco kapelekwa Afrika Kusini katika hospitali ya Netcare Rosebank iliyopo Johannrsburg.
“Nahodha John Bocco leo ameondoka nchini kwenda Afrika Kusini kufanyiwa uchunguzi zaidi wa jeraha la misuli linalomsumbua. Amefika salama na tayari ameanza kupatiwa huduma kwenye hospitali ya Netcare Rosebank iliyopo jijini Johannesburg #NguvuMoja “
VIDEO: Samatta baada ya kupokea comments zinazodai hachezi vizuri Taifa Stars