Saa chache tu baada ya meneja wa zamani wa Liverpool Jurgen Klopp kuteuliwa kuwa mkuu wa shughuli za kandanda za Red Bull, gwiji huyu wa vunywaji vya kuongeza nguvu siku ya Jumatano alihusishwa na kutaka kuinunua klabu ya daraja la pili ya Ufaransa, Paris FC.
Kwa mujibu wa chanzo kinachofahamu suala hilo, mazungumzo yanaendelea kati ya klabu hiyo na Red Bull pamoja na familia ya Arnault wanaomiliki kampuni ya kifahari ya LVMH
Familia ya Arnault na Paris FC walikataa kutoa maoni yao walipoulizwa maswali na AFP.
Rais wa Paris FC tangu 2012, mfanyabiashara na mwenye hisa nyingi Pierre Ferracci, 72, tayari ameelezea nia yake ya kukabidhi hatamu.
Paris FC, inayozidiwa na PSG inayomilikiwa na Qatar katika mji mkuu wa Ufaransa, kwa sasa ipo kileleni mwa Ligue 2 nchini Ufaransa.
Kampuni ya Red Bull ya Austria tayari inamiliki vilabu vya RB Leipzig, Salzburg na New York na inaendesha timu ya Red Bull ya timu inayotawala ya Formula One ya Max Verstappen.–AFP