Mkazi wa Iringa Imani Mfilinge (46) amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kumbaka Mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 13 aliyekuwa akisoma darasa la sita ambapo Mkewe alipomfuma aliendelea kufanya kitendo hicho na alipomaliza akamwambia Mkewe kuwa amepata Mke mwenzie.
Hukumu hiyo imetolewa leo Aprili 24, 2023 na Mahakama Kuu ya Iringa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Rehema Myagilo ambapo kesi imeendeshwa na Mwendesha mashtaka wa Serikali Veneranda Masai.
Mfilinge ametenda kosa hilo Oktoba 11, 2022 ambapo Mtoto wake alitoka Shuleni na kumkuta Baba akiwa nyumbani ndipo akamvutia chumbani huku akimtisha kwa panga wakati Mkewe akiwa msibani na hata Mkewe aliporejea alimkuta Mumewe akiendelea kufanya kitendo hicho na alipomaliza akamwambia Mkewe kuwa amepata Mke mwenzie.