Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuhusika katika makosa mbalimbali ya uhalifu.
Jeshi hilo linamshikilia Anthony Costantine Maningu (50), kwa kumpiga kichwani na kitu kizito na kumsababishia kifo mtoto wake aitwaye Veronica Anthony (17), mwanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Kayenze, Wilaya ya Ilemela Mkoani humo.
Mzazi wa binti huyo, amesema kwamba tukio hilo lilitokea baada ya kile anachokidai kuwa Veronica kurudi nyumbani kwao akiwa amechelewa majira ya usiku kitendo kinachodaiwa kumkasirisha baba yake mzazi na kuamua kuchukua uamuzi huo.