Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga, linamshikilia Masanja Maziku Bugolole (75), mkazi wa Kijiji cha Gula, wilayani Kahama mkoani humo kwa tuhuma ya kumiliki silaha nne aina ya Shotgun, mitutu sita ya Shotgun na risasi 36 kinyume cha sheria.
Taarifa hiyo imetolewa leo Desemba 18, 2020 na Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Debora Magiligimba, ambapo amesema kuwa Masanja alikamatwa Desemba 17, akiwa nyumbani kwake baada ya kufanyika msako maalumu unaoendeshwa na jeshi la polisi la kuwakamata wahalifu mbalimbali.
Alisema kuwa Silaha zilizokamatwa zimebainika kufutika namba zake za uhakiki na zingine zina namba lakini hazijasajiliwa kama sheria za umiliki wa silaha inavyoelekeza, pamoja na kutokuwa na kibali cha kumiliki risasi 36 ambazo alikutwa nazo.
“Kati ya silaha hizo, silaha moja imebainika kuwa na uhakiki wa namba TZCAR 34951, huku usajili wake ukiwa umefutika, ambapo silaha tatu hazina namba za uhakiki bali zina namba za usajili ambazo ni silaha namba D 172321, 14999 na 24162, mtuhumiwa Masanja atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili baada ya uchunguzi kukamilika” Kamanda Magiligimba