Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Hamis Shabani Taletale amewalaumu Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa kudai kuwa hawana msaada wowote kwa wasanii badala yake wamekuwa kama Polisi wa Wasanii.
Taletale ameyasema hayo wakati akichangia mjadala wa makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023.