Kama upo Dar es salaam na huwa unapita barabara ya zamani ya kwenda Bagamoyo najua hili eneo karibu na Shoppers Mikocheni mvua zinaponyesha lazima huwa linakupa kero kwa sababu mvua kidogo tu huwa inahamishia bahari.
millardayo.com imekutana na mbunge wa Kawe Mh. Halima Mdee ambae hili ni eneo lake na anasema ‘Manispaa yetu ya Kinondoni kuanzia mwaka 1995, 2000 na 2005 watu walifanya kama ni shamba la bibi, kila mtu alikua anachuma anachotaka pasipo kujali mipango miji ikoje ama sheria zinasema nini’
‘Matokeo yake ni kwamba yale maeneo ya Shoppers na Tanesco yote yalikua ni maeneo ya mkondo wa maji na kuelekea kule kwa Warioba yalikua ni maeneo ya wazi ambayo maji yalipokua yakitoka huko ukanda mwingine yanapita hapo kuelekea baharini’
‘Sasa Wachakachuzi wa viwanja enzi hizo wakauza haya maeneo na watu wakajenga majengo yao yakaziba mifereji ambayo ilikua imetengenezwa kwa makusudi ya kupeleka maji baharini sasa mvua zikinyesha maji yanajaa, sasa maskini kuna Wananchi wangu wa bonde la mpunga kule yani ndio wanaathirika zaidi pamoja na wapita njia hivyo ikabidi tutafute pesa kupitia mfuko wa barabara na sasa kazi inaendelea’
‘Hii ni project ya kujenga mifereji ya kisasa kwenye eneo hili na itagharimu shilingi BILIONI SITA, sasa u can imagine kama kusingekua na uzembe uliofanyika huko nyuma kwa watu ambao walipewa dhamana ya Kinondoni hii BILIONI SITA ingewezekana ikajenga vibarabara vingi sana vya ndani jimbo la Kawe’
‘Bilioni sita hii itatumika kujenga mifereji mikubwa ambayo itaanzia pale Mikocheni A darajani mpaka huku TANESCO alafu itashuka kuelekea baharini na itasaidia sana Wananchi wangu wa bonde la Mpunga ambao wanateseka sana, inajengwa lami kwa mara ya kwanza barabara ya Maandazi (Maandazi road)’
‘Hii mvua ikiisha na zile project zikiendelea vizuri hiyo miaka ya mbele inayokuja itakwenda vizuri lakini zaidi wote ambao wanatumia barabara ya Bagamoyo ya zamani kwenda Mikocheni, Mabwepande, Kawe na wengine wanaopata mafuriko, kwa ukubwa wa makaravati niliouona naamini itapunguza kero hii kwa muda mrefu, project ya mifereji haitakiwi kuchukua miezi sita ila hii mvua imevuruga mambo mengi sana’
Stori zote ni halali yako kuzipata mtu wangu, ungana na ripota wako wa nguvu kwenye twitter instagram na facebook @millardayo niwe nakutumia kila wakati.