“Napendekeza kupunguza adhabu zinazotolewa chini ya Sheria ya Usalama Barabarani sura 168 kwa makosa ya pikipiki na bajaji kutoka Sh30,000 za sasa hadi Sh10,000 kwa kosa moja. Lengo la hatua hii ni kuweka adhabu kwa kuzingatia uwezo wa kulipa. Aidha, adhabu kwa makosa mengine ya vyombo vya moto zinazotolewa kwa mujibu wa Sheria zinaendelea kubaki kama ilivyo sasa,” Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba.