Mario Balotelli ni mshambuliaji wa Kimataifa wa Italia mwenye asili ya Ghana lakini anaichezea klabu ya Liverpool ya Uingereza, Balotelli wengi tunamfahamu kwa tabia yake ya utukutu huwa haoni hatari kufanya jambo lolote liwe zuri au baya maadam akili yake imemtuma kufanya atafanya tu.
August 6 nakuletea mkusanyiko wa matukio mbalimbali aliowahi kuyafanya ambapo kwa tabia yake ya utukutu ni kawaida kuona kafanya vitendo hivyo, nakuletea mkusanyiko wa matukio ya kijinga aliowahi kuyafanya Balotelli .
1. Mwaka 2013 aliwahi kukunjana na kocha wake Roberto Mancini ambae ndiye kocha namba moja anaeongoza kuvumilia kwa vituko vyake yaani kwa maana nyingine mtaani huwa wanatania Mancini ni kama baba wa Balotelli kwa aina ya makocha kama Sir Alex Ferguson na Louis van Gaal wasingeweza kuvumilia vituko vyake.
2. Mwezi March 2011 alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kucheza faulo mbaya na ya kijinga kwa mchezaji wa klabu ya Dynamo kiev katika mchezo wa Europa Ligi.
3. Ni mtu mwenye vituko na maudhi mengi kwa baadhi ya watu wanaomzunguuka kwani kama wewe sio mtu mwenye subira utakwazika, alishindwa kuvaa bib ili afanye mazoezi ya kupasha misuli moto hadi moja kati ya viongozi wa benchi la ufundi alipokuja kumvalisha.
4. Aliwahi kutolewa Uwanjani baada ya kukosa goli la kizembe baada ya kuwa katika nafasi nzuri ya kufunga kwa zaidi ya asilimia 90 lakini alifanya mzaha na kutoa mpira nje, ilikuwa ni katika mchezo wa maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Uingereza mchezo kati ya Man City dhidi ya L.A Galaxy.
5. Kama kawaida yake hufanya matukio usio yatarajia basi aliwahi kumrumshia mshale wa dats mchezaji wa timu B ya Manchester City na kupigwa faini ya pound 100,000/= alipoulizwa kwa nini alifanya vile jibu lake lilikuwa rahisi sana aliniudhi bila kupima uzito wa kosa na kitendo alichomfanyia da!!! huyo ndio Balotelli bwana.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos