Raundi ya pili ya mechi za makundi ya kombe la dunia inaelekea ukingoni huku mataifa makubwa kwenye soka kama Spain, England, Ureno, na Italy wakipokea vipigo kutoka kwa timu zisizo na mastaa wakubwa kwenye timu zao.
Usiku wa jana tulishuhudia Costa Rica wakiendelea kuishangaza dunia kwa kutoa vipigo kwa timu kubwa, baada ya kuiadhibu Uruguay kwenye mechi ya kwanza, jana ilikuwa zamu ya Italia. Goli pekee la Bryan Ruiz anayeichezea Fulham liliizamisha Azzuri waliokuwa wakiongozwa kijana mtukutu mshambuliaji Mario Balotelli.
Ushindi wa Costa Rica sio tu umeiweka pabaya Italy bali pia umemkosesha zawadi ya mabusu Mario Balotelli.
Balotelli juzi usiku baada ya England kufungwa na Uruguay alitweet kwamba endapo Italia wataifunga Costa Rica na kuisadia England kuendelea kubaki kwenye mashindano, basi angetaka apewe zawadi ya mabusu kutoka kwa Malkia wa Uingereza Queen Elizaberth.
Lakini kutoka na kufungwa kwa Italy – England imeungana na Spain, Australia, Cameroon kuwa miongoni mwa timu za kwanza kuaga mashindano hayo.