Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt. John Simbachawene, amevitaka vyombo vya habari vya nchini Kenya kuripoti taarifa zenye uhakika kuhusu Tanzania na kuacha kutoa maneno yenye kuleta hofu kwa watu.
Balozi Simbachawene ametoa kauli hiyo ofisini kwake Jijini Nairobi nchini Kenya, baada ya chombo kimoja cha habari nchini Kenya kuripoti taarifa za uwepo wa taharuki za ugonjwa wa Corona nchini Tanzania jambo ambalo si la kweli.
Mbali na hayo Balozi Simbachawene, amewataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari za COVID-19, na kueleza kuwa Tanzania imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wanafuata ushauri wa wataalamu na Wizara ya Afya pamoja na miongozo inayotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Aidha, ametoa raia kwa Tanzania wanaotaka kwenda nchini Kenya kuhakikisha wana nyaraka hitajika kwa mujibu wa Wizara ya Afya, na wale wanaoishi nchini humo amewasihi kufuata kanuni na masharti yaliyowekwa kupambana na ugonjwa wa COVID-19.
MTANZANIA AUNDA MAGARI, CROWN ATHLETE IPO, ANAPIGA HELA “WAZUNGU WANANUNUA”