Kutoka nchini Kenya, gumzo limezuka leo May 4, 2018 baada ya wananchi kuharibu bango la matangazo lenye maandishi ya lugha ya Kichina lililokuwa katika barabara Kuu ya Mombasa kwenda Nairobi.
Inadaiwa kwamba wananchi walikerwa na kulalamikia uwepo wa bango hilo kuwa na lugha ambayo haileweki na wazawa tena bila hata kuwekewa tafsiri ya Kiswahili au Kiingereza.
Baadhi yao waliwaomba maafisa wakuu wa serikali wawasaidie kutafsiri bango hilo.
Inaelezwa kuwa ni namba za simu tu zilizopo kwenye bango hilo ndizo zimeandikwa kwa Kirumi.