Afisa wa benki ya NatWest ameshtakiwa kwa kosa la kuuza taarifa za wateja kwa kundi la wahalifu ambapo amehurumiwa kufungwa gerezani kwasababu ana watoto wadogo wawili.
Lekeshia Henry-Richards, 28, aliiba sahihi za wateja 150 waliokuwa wakitumia huduma binafsi katika jiji la London.
Taarifa hizo zilitumika kuwaibia wateja ambapo wateja kadhaa wameibiwa kupitia kundi hilo la kihalifu kabla ya ishu nzima kugundulika April mwaka huu na mwanamke huyo kufikishwa mahakamani.
Mwanamke huyo kutoka Leytonstone, Mashariki mwa London alisamehewa kufungwa gerezani kwasababu ana watoto wadogo wawili mmoja mwenye miaka minane na mwingine miezi 18.
Alihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani na kuagizwa kufanya kazi kwa saa 90 bila malipo.
Unataka kupata story kama hizi zikufikie popote ulipo?, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB