Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Adam Malima amemtaka mkandarasi anayesimamia mradi wa ujenzi wa barabara ya kidatu – ifakara yenye urefu wa kilomita 66.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami na daraja la Ruaha kufanya kazi usiku na mchana kuwezesha kukamilika kwa wakati.
Akizungumza mara baada ya kutembelea na kujionea hali halisi ya ujenzi wa barabara na daraja hilo Rc Malima amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutafungua uchumi wa wananchi wa wilaya za Kilombero,Malinyi na Ulanga.
Mradi wa ujenzi wa barabara hiyo unafadhiriwa na mfuko wa maendeleo wa nchi za Ulaya(European Development Fund EDF) ukishirikiana na Shirika la Msaada wa Uingereza (UKAID) na Shirika la Kimarekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rc Malima amesema mradi huo utakapo kamilika unategemewa kuinua maisha ya mtu mmoja mmoja hasa wakulima wa bonde la mto kilombero ,uwekezaji uchimbaji madini Wilaya ya Ulanga.
Kwa upande wake mhandisi mkazi TANRODS Arnod Maeda amesema ujenzi mradi wote kwa ujumla barabara na daraja la Ruaha umefikia asilimia 82.8 na unatarajiwa kukamilika mwezi machi 2024 na unatarajiwa kugharimu zaid ya shilingi Bilion 128.