Baraza la Wawakilishi linataraji kupiga kura leo Jumatano kupeleka mashtaka dhidi ya Rais Donald Trump mbele ya Bunge la Seneti ikiwa ni hatua ya mwisho kabla ya kuanza kwa kesi ya kumuondoa Rais huyo madarakani.
Spika wa Baraza hilo, Nancy Pelosi, ametangaza kwamba mashtaka yanayomkabili Donald Trump yatapelekwa mbele ya Bunge la Seneti leo Jumatano.
Donald Trump anakabiliwa na mashtaka ya Matumizi Mabaya ya Madaraka na kuzuia Bunge kufanya shughuli zake.
Upinzani unaamini kwamba, Rais Donald Trump alitumia rasilimali za Serikali kushinikiza Ukraine kumchunguza aliyekuwa Makamu wa Rais kutoka Democratic, Joe Biden.
AWESO ACHONGEWA NA WANANCHI KWA BASHIRU KISA KUZINGUANA NA MKANDARASI