Baraza la mawaziri la Israel siku ya Jumapili walianza kile kinachotarajiwa kuwa kikao cha kuidhinisha bajeti iliyorekebishwa ya 2024 ili kuelezea ongezeko kubwa la matumizi ya fedha kufadhili vita vya nchi hiyo na kundi la waislamu wa Palestina Hamas.
Kwa kawaida, majadiliano hudumu hadi usiku na huenda kura isifanyike hadi alfajiri ya Jumatatu.
Israel mwaka jana iliidhinisha bajeti ya miaka miwili ya 2023 na 2024, lakini vita dhidi ya Hamas huko Gaza vimetikisa fedha za serikali, vinavyohitaji mabadiliko ya bajeti na matumizi ya ziada.
Mabilioni ya shekeli katika fedha za ziada zinahitajika ili kufadhili jeshi, kufidia askari wa akiba na makumi ya maelfu ambao wanaishi karibu na mpaka na wamekimbia makazi yao, pamoja na wale walioathirika moja kwa moja na mashambulizi ya Oktoba 7 ya wapiganaji wa Hamas.
Hata hivyo, bajeti hiyo imekuwa ya kisiasa na yenye utata, hasa kuhusu malipo Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alikubali chini ya mkataba wa muungano wa 2002 na Waziri wa Fedha Bezalel Smotrich na wakuu wa vyama vingine vya kidini.