Edward Lowasa, ametunukiwa Tuzo ya Baraza la Mawaziri wa Maji Afrika (AMCOW).
Tuzo hiyo imetolewa jana Jumanne, jijini Dakar, Senegal na Waziri wa Maji wa Nigeria, Suleiman Adam ambapo imepokelewa na Fredrick ambaye ni mwanae.
Fredrick akizungumza kwenye baraza hilo ambalo baba yake ni miongoni mwa waasisi wake, alisema “niko hapa leo kupokea tuzo kwa niaba ya baba yangu, ni bahati mbaya hayuko vizuri kwa sasa, amelazwa hospitali lakini tunaamini kwa maombi yenu ataamka tena na kulitumikia taifa lake.”
Amesema, baba yake kipaumbele chake kikuu kilikua maji na elimu, jambo lililomsukuma kwenye wakati wake akiwa kama Waziri wa Maji kwenda Nnchini Misri kupigania matumizi ya maji ya ziwa viktoria kwa wote ili kukomboa wakina mama ambao leo hii kwa jitihada hizo zaidi ya vijiji 500 kanda ya ziwa ni wanufaikaji wa maji hayo.