Ni Julai 18, 2023 ambapo Baraza la Michezo la Taifa (BMT) lilikutana na vyombo vya habari kuzungumzia uboreshwaji ama mipango yako katika sekta ya michezo.
Baraza hilo linasema chombo kilichoundwa kisheria ili kusimamia na kuendeleza michezo nchini imeendelea kufanya kazi zake kwa kusimamia Sheria pamoja na taratibu ilizojiwekea kuhakikisha kuwa michezo inaendelea kustawi na kupiga hatua zaidi kuliheshimisha Taifa hususan katika mashindano ya Kimataifa.
Katika Serikali ya awamu ya sita inavoongozwa na Rais mchapakazi na mpenda michezo Mheshimiwa Dokta Samia Suluhu Hassan, kupitia Wizara yene dhamana ya michezo.
Baraza la Michezo la Taifa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 limetekeleza
– majukumu vafuatayo;
1. Baraza limeweza kuzigharamia Timu za Taifa kushiriki katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa, ambapo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023, Baraza limetumia takribani shilingi Bilioni Nne nukta mbili (4.2B) kuziwezesha timu kushiriki katika mashindano va Kimataifa. Timu zilizowezeshwa ni pamoja na:-
(M) Riadha, Ngumi, Judo, Kuogelea, Baseball, Kabaddi, Tenis, Mpira wa Miguu, Netiboli na Kunyanyua Vitu Vizito kwa Walemavu;
Timu ya Tanzania iliwezeshwa kushiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola yalivofanvika Birmingham nchini Uingereza mwaka 2022 ambapo katika machindano hayo Tanzania lipata jumla ya medali tatu katika mchezo wa Riadha na Ngumi;