Mataifa wanachama wa Shirika la Afya Ulimwenguni Jumatatu yaliidhinisha bajeti ya dola bilioni 6.83 kwa miaka miwili ijayo ambayo inajumuisha nyongeza ya 20% ya ada zao za lazima.
Pendekezo la bajeti ya 2024-2025 lilipitishwa bila pingamizi na lilipongezwa kwa muda mrefu.
Mkurugenzi Mkuu Tedros Adhanom Ghebreyesus alielezea hatua hiyo kama “ya kihistoria na hatua kubwa”.
Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, alipongeza hatua hiyo kama kwa kuita ya kihistoria na hatua kubwa.
Bajeti hiyo bado inahitaji kuidhinishwa na nchi zote wanachama mwishoni mwa tukio hilo la siku 10 lakini utaratibu wa kuidhinisha kimsingi ni kwa ajili ya utaratibu tu.
Uamuzi huo umefanyika baada ya mkutano wa mwaka jana kukubali kufanya marekebisho makubwa ya ufadhili wa WHO.
Baada ya kusumbuliwa na janga la COVID-19, mataifa yalikubaliana juu ya uhitaji wa kutoa ufadhili wa kuaminika na wenye uthabiti.
WHO inafadhiliwa kwa kiasi kikubwa na nchi wanachama 194.
Sehemu ya ufadhili kutoka ada ya lazima ya uanachama yaani michango iliyokadiriwa ilipigiwa hesabu kulingana na utajiri na idadi ya watu ilipungua mpaka chini ya moja ya tano na iliyobaki ikitoka kwa michango ya hiari.
Mkutano wa mwaka jana ulikubali kuongeza hatua kwa hatua sehemu ya ada ya wanachama hadi asilimia 50 itakapofikia bajeti ya 2030 – 2031.