Barcelona wamejiunga na orodha inayokua ya vilabu vinavyohitaji kumnunua kiungo wa kati wa Manchester City Kalvin Phillips, 28, kulingana na theTelegraph.
Miamba hao wa Uhispania wanaungana na Atletico Madrid, Crystal Palace, West Ham, Newcastle na Juventus ambao wote wanawania saini ya Phillips.
Inakuja huku ripoti kwamba Newcastle wanatafuta kiungo barani Ulaya iwapo Phillips hawezi kuishawishi klabu yake kupunguza ada yake ili aondoke kwa mkopo.
Iwapo Tottenham itaamua kumuuza kiungo wake wa kati wa Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, klabu ya Italia Napoli itamnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, kulingana na Telegraph.
Mwandishi wa habari wa Kiitaliano Fabrizio Romano anaripoti kuwa Tottenham inatafuta kumsafirisha Japhet Tanganga, ambaye anaelekea kujiunga na Millwall hadi mwisho wa msimu.