Barcelonawamefanikiwa kutengeneza rekodi kadhaa usiku wa leo katika ligi kuu ya Hispania baada ya kupata matokeo chanya dhidi ya Rayo Vallecano kwenye dimba la Estadio del Rayo Vallecano.
FC Barcelona ilifanikiwa kushinda mechi hiyo kwa ushindi wa magoli 2-0 – Messi na Neymar wakifunga magoli hayao.
Kufuatia ushindi huo wa 2-0, Barca imefanikiwa kuweka rekodi ya nzuri kwenye safu ya ulinzi.
Kikosi cha Luis Enrique sasa kimefanikiwa kuwa timu ya kwanza katika historia ya La liga kucheza mechi 7 za mwanzoni mwa ligi hiyo bila kuruhusu wavu kugushwa.
Pia wakati huo huo golikipa wa timu hiyo, Mchile Claudio Bravo ameweka rekodi mpya ya katika kulinda lango lake.
Bravo amevunja rekodi ya kucheza dakika nyingi bila kuruhusu wavu wake kuguswa, mpaka kufikia sasa Bravo amecheza jumla ya dakika 561 bila kufungwa goli, akivunja rekodi ya golikipa wa zamani wa Barca, Pedro Artola aliyecheza kwa dakika 560 bila kufungwa goli katika msimu wa 1977-78.