Baada ya katikati ya wiki kupata ushindi wa 5-4 dhidi ya Sevilla katika mchezo wa UEFA Supercup, klabu bingwa ya ulaya FC Barcelona leo wamekutana na kipigo kizito kutoka kwa Athletic Bilbao.
Vilabu hivyo vilivyocheza fainali ya kombe la mfalme wa Hispania msimu uliopita, leo vilikutana kwenye mchezo wa Spanish Supercup ambao umemalizika kwa Barca kufungwa magoli 4-0.
Kiungo San Jose alifungua akaunti ya magoli ya Bilbao katika dakika ya 14 – goli lilodumu mpaka kipindi cha kwanza kilipomalizika.
Kipindi cha pili Bilbao walicharuka na kufunga magoli mengine matatu kupitia mshambuliaji hatari Aduriz, aliyefunga katika 53, 62, na dakika ya 68.
Timu hizo zitarudiana wiki mbili zijazo katika dimba la Nou Camp.