Barcelona wamempa kiungo Frenkie de Jong chaguzi ya vilabu kadhaa vikubwa vya Ulaya huku mashaka yakibaki juu ya utimamu wake kiafya, kwa mujibu wa Sport.
De Jong, 26, anaweza kufanyiwa upasuaji kutokana na jeraha la kifundo cha mguu ambalo lilimfanya kukosa Euro 2024 akiwa na Uholanzi, na huenda akakaa nje ya uwanja kwa miezi michache zaidi.
Barca wameanza msimu vizuri bila yeye na wameshinda mechi nne mfululizo, lakini uhusiano wa mchezaji huyo na rais wa klabu Joan Laporta unaripotiwa kuwa mbaya.
De Jong hadi sasa amekataa kuuzwa, lakini mara tu atakaporejea katika utimamu wake kamili inaonekana klabu ina nia ya kutafuta mchumba, huku Man United wakiwa wanahusishwa zaidi.