Barcelona wanamfikiria kiungo wa kati wa Ufaransa N’Golo Kanté kama mchezaji anayetarajiwa kusajiliwa msimu huu wa joto, Diario Sport inaripoti.
Kante, 33, alijiunga na Al Ittihad ya Saudi Arabia msimu uliopita wa joto kwa uhamisho wa bure baada ya mkataba wake na Chelsea kumalizika.
Hata hivyo, amedokeza angependa kurejea kucheza Ulaya na kuna vilabu kadhaa, vikiwemo Barca, West Ham na Atletico Madrid, vinavutiwa na huduma yake.
Mkurugenzi wa michezo wa Barca Deco amekuwa akimpenda Kanté, ambaye alikuwa mmoja wa wachezaji bora wa Ufaransa kwenye Euro 2024, na hatua hiyo inaweza kuwa chini ya vigezo vyao vya kifedha.