Wakati wapinzani wao wa jadi Real Madrid wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 4-1 dhidi ya Getafe na kuvuna point zote tatu katika dimba la Santiago Bernabeu, FC Barcelona wao walilazimika kusafiri hadi katika dimba la Mestalla kucheza na Valencia katika mchezo wao wa 14 wa Ligi Kuu Hispania msimu wa 2015/2016.
Mchezo wa FC Barcelona dhidi ya wenyeji wao Valencia haukuwa mwepesi, tofauti na wengi walivyokuwa wanatarajia, kwani katika mechi zake nne FC Barcelona ilizocheza hivi karibuni imefanikiwa kufunga jumla ya magoli 20 na kuweka wastani wa ushindi wa goli tano kwa kila mechi.
Dimba la Mestalla linaonekana kuwa gumu kwa FC Barcelona kwani wameshindwa kupata ushindi na kuwambulia sare ya kufungana goli 1-1. Licha ya Valencia kutajwa kuwa safu ya ulinzi imara, Luis Suarez alifanikiwa kufunga goli la kuongoza dakika ya 59, kabla ya Santi Mina kuisawazishia Valencia dakika ya 86.
Video ya magoli ya Valencia Vs FC Barcelona
https://youtu.be/116W8zaiZ4U
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.