Tunafahamu ndugu zetu Kagera walipatwa na maafa ya tetemeko la ardhi, baadhi yao walifariki na wengine kukosa makazi.
Hivi karibuni tumepata kauli ya serikali akiwemo rais Magufuli kuwataka wananchi hao wa Kagera kujisimamia wenyewe katika kurejesha makazi yaliyoharibiwa na tetemeko hilo tukaona baadhi ya watu wakiandika kwenye mitandao ya kijamii kukosoa hatua hiyo ya serikali.
Lakini hatujasikia upande wa wananchi wenyewe wa Kagera wanasema nini…
Millardayo.com imempata mbunge wa Kagagwe, Kagera ambaye ni muwakilishi wa wananchi na ana haya ya kusema….
‘Ni kweli serikali haiwezi kumsaidia kila mmoja kwasababu wahanga ni wengi, wananchi wamelielewa kwakuwa ni jambo ambalo hakuna aliyelitegemea lakini tungeiomba serikali ingewasaidia wananchi punguzo la vifaa vya ujenzi ili kuwasaidia wananchi‘ –Innocent Bashungwa
‘Wananchi wamemuelewa Rais Magufuli na serikali kwa ujumla ingawa ni vyema wakapewa baadhi ya misaada inayowezekana‘ –Innocent Bashungwa
Kuna wananchi hadi sasa bado wanalala nje kutokana na kukosa makazi? Bashungwa amesema ‘Kwasasa hakuna mwananchi analala nje kwa kukosa msaada, zaidi tuwasaidie mahitaji yao muhimu likiwepo hilo la makazi‘ –Innocent Bashungwa
‘Kwa upande wa Karagwe kuna tatizo la ukame na kusababisha njaa karibu wilaya nzima hivyo niiombe serikali iweke punguzo la bei ya vyakula hasahasa mahindi na maharage bila kusahau punguzo la pembejeo‘ –Innocent Bashungwa
Unaweza kuendelea kumsikiliza hapa mbunge Innocent Bashungwa
MBUNGE BASHUNGWA ‘MUDA HAUKUTOSHA KUELEZEA KAULI YA WANAUME KUSHINDWA KUOA WANAWAKE WAZURI’