WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe amesema mauzo ya nafaka nje ya nchi yameongezeka kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji nchini.
Bashe ameyamesemwa leo tarehe 8 agosti 2023 katika kilele cha Maonesho ya Kimataifa ya Nane Nane, yaliyofanyika kitaifa jijini Mbeya.
Waziri Bashe amesema majuzi ya mahindi nje ya nchi yameongezeka kutoka tani 223,000 msimu wa mwaka 2021/2022 hadi tani 415,000 mwaka 2022/2023 huku mchele uliouzwa nje ya nchi ukifika tani 352,000 ilihali mchele wameuza tani 352,000 katika msimu wa 2022/2023.
Bashe pia amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ruzuku ya kuwapatia pembejeo za kupulizia fangasi kwenye parachichi na kupelekea parachichi ya Tanzania kuwa na daraja la pili kwenye soko la Kimataifa.
Bashe ameongeza kuwa parachichi aina ya HASS inayozalishwa Tanzania imepata rekodi bora kuliko parachichi zote zinazozalishwa katika Afrika Mashariki na kuongeza kuwa uzalishaji umeongezeka kutoka tani 9000 hadi 29,031 msimu wa kilimo uliopita.