Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa ametembelea kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu waenezao Malaria (Tanzania Biotech product limited – TBPL) kilichopo chini Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kilianzishwa kwa ushirikiano wa nchi ya Cuba baada ya nchi hiyo kukubaliana kupitia Tanzania teknologia ya kuzalisha viuadudu.
Viuadudu ni bidhaa za kibailojia ambazo hutumika kuua viluwiluwi wa mbu waenezao ugojwa wa malaria, dengu na mabusha. Kwa sasa kiwanda kinazalisha aina mbili za viuadudu ambavyo ni Griselesf na Bactivec.
Bashungwa baada ya kufika kiwandani hapo aliomba kupewa taarifa ya utekerezaji wa maelekezo aliyoyatoa mwezi January mwaka jana alipotembelea kiwanda hicho kuwa kiwanda kianze kutengeneza viuatilifu kwa ajili ya zao la pamba na korosho, ambayo mpaka sasa hayajatekelezwa.
“Mkakati wa serikali ni kuboresha kiwanda hiki ili kiweze kutusaidia kupambana na malaria pia kwa wakulima wa pamba na korosho, Mimi nilikuja hapa January 4 2019 nikauliza kiwanda hiki si kinaweza kutengeneza viuatilifu kwa ajili ya pamba na korosho, nyie wenyewe mkasema inawezekana kabisa” Bashungwa
“Hatuhitaji kuongeza jengo wala mitambo mingine na nikatoa magizo kwamba ndugu zetu wa Cuba kwa sababu nyie ndo mnatoa teknolojia, boresheni ili tuanze kutengeneza viuatilifu kwa ajili pamba, lakini mpaka sasa hakijafanyika kitu” Bashungwa
“Maana pamba peke yake nchini kila msimu tunatumia kiasi kisichopungua bilioni 40 kuagiza viuatilifu kutoka nje na kwenye korosho bilioni 30, kwa hivyo tu wiwili tunatumia bilioni 70 kila msimu kuagiza kutoka nje, zingekuwa zinakuja hapa kiwanda kinafanya hiyo kazi maana soko lipo” Bashungwa
Bashungwa baada ya kusomewa taarifa na kutoridhishwa na mwenendo na utendakaji wa wabia kutoka Cuba amesema iandikwe barua kwa Wizara ya Mambo ya Nje ili waiandikie barua Wizara ya Viwanda ya Cuba kuwa hii timu haitufai waje watu wengine.
“Kiwanda hiki NDC wewe una ubia 100% na hawa watu wanatupa teknologia tu, kwa vile tumeshaona watu hawa hawatufai, Katibu Mkuu inabidi tuwasiliane na Mambo ya Nje hawa watu hawatufai, hii timu iondoke walete timu nyingine ambayo itashirikiana na serikali kuendesha kiwanda” Bashungwa
LEMA AMJIBU KAMANDA WA ARUSHA “HANA MAMLAKA YAKUNIONYA, AJE ANIKAMATE”