Ni habari za leo May 25 2017 mchana kutokea upande wa kanda ya ziwa ambako bado Wakazi wa eneo hilo hawajasahau tetemeko lililogharimu maisha ya watu na mali zao kwa upande wa Kagera.
Habari ya leo ni kwamba tetemeko limeripotiwa kutokea hukohuko Kanda ya ziwa kwenye maeneo ya Mwanza na Geita lakini hakuna madhara yaliyoripotiwa mpaka sasa.
Japo halijasababisha uharibifu wowote tetemeko hilo la leo ambalo inaripotiwa limechukua kuanzia sekunde 7-10 limesababisha baadhi ya waliokuwemo kwenye majengo ya gorofa kutoka kwenye majengo hayo wakiwemo Wanafunzi wa SAUT Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera hivi karibuni alisema matetemeko madogomadogo yanayopita kwa muda mfupi ni vizuri yakatokea kwasababu yanasaidia miamba kupumua, ni afadhali hayo yakatokea kidogokidogo kuliko yale yanayochukua miaka kutokea lakini yakitokea yanakua makubwa na yanasababisha madhara.
VIDEO: Hii kali, Mchungaji aliyeoa Mke wa muumini wake Kagera, tazama Mkuu wa Wilaya alivyofika na kuwahoji