Ingawa hakuna tangazo rasmi lililotolewa, Paris Saint-Germain imeripotiwa kuongeza mchezaji mwingine kwenye kikosi chake ambaye anafaa kusaidia kwenye safu ya ulinzi na kwa mujibu wa Fabrizio Romano, mwandishi habari za michezo anasema FC Bayern Munich imekubali kumuuza Lucas Hernández kwa PSG kwa kitita cha jumla ya €48-€50 milioni.
Romano pia anaripoti kwamba Hernández atasaini rasmi mkataba na PSG leo ambao utamweka klabuni hapo hadi 2026.
Ni hatua ya kushangaza kwa PSG ,Hernández bado anauguza jeraha ambalo lilimlazimu kukosa mechi 25 msimu uliopita akiwa na Bayern.
Ikiwa Hernández anaweza kuwa na afya njema, hii inaweza kuwa hatua nzuri kwa PSG.
Hernandez ataondoka Bayern baada ya miaka minne katika klabu hiyo, baada ya kujiunga na Atletico Madrid mwaka wa 2019.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye alipitia akademi ya Los Colchoneros, aliuzwa kwa ada ya rekodi ya klabu wakati huo ya €80m. .
Dili la PSG kwa Hernandez litakuwa na thamani ya euro milioni 50, ambayo ni habari njema kwa Atletico kwani wako katika mstari wa kulipwa zaidi.